Dkt Chamriho awa Mwenyekiti wa Bodi

0
190

Rais John Magufuli amemteua Dkt Leonard Chamriho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Uwekezaji wa Mapato ya Mafuta na Gesi.

Dkt Chamriho ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti huyo, Rais Magufuli amewateua Wajumbe Wanne wa Bodi hiyo ya Ushauri ya Uwekezaji wa Mapato ya Mafuta na Gesi ambao ni Casmir Kyuki ambaye ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Suleiman Missango ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Wajumbe wengine ni Safiel Msomvu ambaye ni Kaimu Meneja Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na
Dkt Mussa Budeba ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa, uteuzi wa Dkt Chamriho na Wajumbe hao Wanne wa Bodi hiyo ya Ushauri ya Uwekezaji wa Mapato ya Mafuta na Gesi umeanza Septemba 25 mwaka huu.