Watu 25 wamekufa na wengine zaidi ya Mia Moja wamejeruhiwa, baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa Nane katika vipimo vya matetemeko -Ritcha kuitikisha Pakistan.
Tetemeko hilo la ardhi limelitikisa eneo kubwa la jimbo la Kashmir linalodhibitiwa na Pakistan.
Habari kutoka nchini Pakistan zinasema kuwa, tetemeko hilo pia limeharibu majengo kadhaa na njia mbalimbali za mawasiliano ikiwa ni pamoja na barabara.