Dkt Msengwa Mwenyekiti Bodi ya NBS

0
177

Rais John Magufuli amemteua Dkt Amina Msengwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Dkt Msengwa ambaye ni Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Takwimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Andrew Massawe aliyemaliza muda wake.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa, uteuzi wa Dkt Msengwa umeanza Septemba 19 mwaka huu.