Shirika la Afya Duniani (WHO) limesisitiza kuwa halijawahi kusema na wala halina ushahidi wowote kuwa Tanzania kuna ugonjwa wa Ebola.
Kauli hiyo imetolewa hii leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa WHO nchini Dkt Tigesti Ketsela Mengustu wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
Wakati wa mazungumzo yao Dkt Mengustu na Dkt Ndumbaro wamejadili kuhusu uchunguzi wa ugonjwa wa Ebola nchini.
WHO imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali.