Rais Magufuli amewataka viongozi kutatua kero za wananchi

0
132

Rais John Magufuli amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi hao akiwemo Mkuu mpya wa mkoa wa Morogoro, -Loata Sanare, Rais Magufuli amemtaka kwenda kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa huo.

Amesema kuwa, hajaridhishwa na namna uongozi uliopita wa mkoa huo chini ya Dkt Stephen Kebwe ulivyokua ukitekeleza majukumu yake na ndio maana akaamua amuondoe madarakani.

Ameongeza kuwa, mkoa wa Morogoro umejaa matatizo mengi ambayo hayajashughulikiwa kwa muda mrefu, na ambao baadhi ya viongozi wake wamekua wakitumia mapato ya serikali kwa matumizi binafsi, hivyo ni vema Mkuu mpya wa mkoa huo akayashughulikiwe matatizo hayo kwa haraka na bila upendeleo.