Laini Milioni Tano tu za simu zasajiliwa hadi sasa

0
191

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeeleza kusikitishwa na mwitikio mdogo wa Wananchi katika kusajili laini za simu za mkononi kwa kutumia alama za vidole.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano kwa Umma kutoka TCRA,- Fredrick Ntobi amesema kuwa, hadi kufikia mwezi Agosti mwaka huu, ni laini Milioni Tano tu za simu ndizo zilizokua zimesajiliwa kwa mfumo huo.

Zoezi hilo la kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole linatarajiwa kukamilika Disemba 31 mwaka huu.