Akothee akumbana na kizuizi Bungeni

0
2141

Msanii wa muziki na mfanyabiashara nchini Kenya, #Akothee amekutana na kizuizi cha walinzi katika eneo la majengo ya Bunge kutokana na aina ya mavazi yake aliyovaa

Akothee alifika Bungeni hapo kwa mwaliko wa Mbunge David Sankok, alizuiwa kwa takribani dakika 20, baadae aliruhusiwa kuingia katika Mgahawa wa eneo la Bunge baada ya kujistiri kwa leso iliyotoka kwa Afisa mwanamke aliyekuwa katika eneo hilo.

Hata hivyo, Akothee alisikika akisisitiza juu ya mavazi yake kuwa ndo uvaaji wake tofauti na alivyotakiwa kuvaa ili aweze kuingia eneo hilo.