Kura zaanza kuhesabiwa Israel

0
823

Zoezi la kuhesabu kura limeanza nchini Israel, baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu nchini humo, uchaguzi uliofanyika kwa mara ya pili katika kipindi cha mwaka huu, baada ya serikali kushindwa kuunda Serikali na uchaguzi kulazimika kurudiwa.

Serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, -Benjamin Netanyahu ilishindwa kuunda serikali kwa vile chama chake cha LIKUD hakikupata viti vya kutosha na upande wa upinzani ulioahidi kuungana naye kukataa Muungano huo.

Hata hivyo habari kutoka nchini Israel zinasema kuwa, huenda kukawa na mchuano mkali na huenda pia asipatikane mshindi wa moja kwa moja ambaye chama chake kinaweza kuunda serikali.

Netanyahu ameahidi kuwa, endapo atachaguliwa kuliongoza Taifa hilo, ataunda Serikali yenye mshikamano na hatakuwa tayari kushirikiana na vyama vyenye misimano ya Kiarabu.