Moto umeteketeza baadhi ya majengo katika Shule ya Sekondari ya Old Tanga iliyopo mkoani Tanga.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, -Edward Bukombe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, moto huo umeteketeza majengo mawili ambalo ni la mikutano na lingine la kuhifadhia vifaa.
Hata hivyo Kamanda Bukombe amesema kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na polisi wanaendelea na uchunguzi.