Tayari nimefanyiwa baadhi ya vipimo : Kabendera

0
155

https://www.youtube.com/watch?v=KiosslOouOg&feature=youtu.be

Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi Erick Kabendera, kwa mara nyingine tena hii leo, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.

Kabendera anayekabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi, alifika Mahakamani hapo akiwa bado anatembea kwa kuchechemea na kusema kuwa jana kwa mara ya kwanza alipelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Amana iliyopo jijini Dar es salaam na kupimwa afya yake.

Ameiambia Mahakama kuwa, tayari amefanyiwa kipimo cha X-Ray na majibu ya awali yameonesha kuwa ana tatizo la mgongo.

Kabendera ameongeza kuwa, kipimo kingine alichofanyiwa ni cha damu na majibu yake yanaweza kuwa tayari mwisho mwa wiki hii huku akibainisha kuwa bado anapata maumivu makali ya mgongo.

Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba Mosi mwaka huu, baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi haujakamilika lakini upo katika hatua nzuri.