Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imezindua Kituo cha kuhifadhi na kusambaza fedha mpya katika Benki ya NMB Tawi la Mkwawa lililopo mjini Iringa.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki Kuu mkoani Mbeya, – Ibrahim Malogoi amesema kuwa hatua hiyo ina lengo la kupunguza mzunguko wa fedha chakavu kwa Wakazi wa mkoa huo ambazo zinaongeza hatari ya kutengenezwa fedha bandia.
Malogoi amesema kuwa BOT imesikia kilio cha Wafanyabiashara wa Iringa ambao kwa muda mrefu wamelalamika uwepo wa fedha zilizochakaa kutoka benki nyingine.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, – Ally Hapi ameishukuru Benki Kuu kwa kuzindua kituo hicho ambacho kitarejesha hadhi ya fedha na kupunguza mzunguzo wa fedha zilizochakaa.