Makamu wa Rais atia saini kitabu cha maombolezo

0
203

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, leo amefika katika ofisi za Ubalozi wa Zimbabwe nchini zilizopo jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kutia saini kitabu cha maombolezo, kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa
nchi hiyo Mzee Robert Mugabe, kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita
nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu.

Katika Salamu zake za pole kwa Raia wa Zimbabwe, Makamu wa Rais amewataka wawe na subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha maombolezo pamoja na maandalizi ya mazishi ya kiongozi huyo.