TFF na Azam Media wasaini mikataba miwili

0
1069

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kampuni ya Azam Media, leo wamesaini mikataba miwili ya muda wa miaka Minne.

Mikataba hiyo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni Sita ni kwa ajili ya udhamini wa mashindano ya Azam Sports Federation Cup na pia kuonyesha mechi za timu ya Taifa.