Majeruhi wa ajali ya moto waruhusiwa

0
154

Majeruhi Watatu kati ya Kumi na Moja waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam, kufuatia ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro wameruhusiwa hii leo.

Mkuu wa kitengo cha uhusiano wa hospitali hiyo Aminiel Aligaesha amethibitisha kuruhusiwa kwa majeruhi hao.

Ajali hiyo ya moto iliyotokea Agosti Kumi mwaka huu baada ya lori la mafuta kupinduka na baadaye kuwaka moto mkoani Morogoro, ilisababisha vifo vya zaidi ya watu Mia Moja.