Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa, Serikali imenzisha Kituo cha Pamoja kwa ajili ya kuwahudumia Wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi, kituo kitakachowawezesha kupata huduma kwa haraka na kuwekeza nchini.
Amesema kuwa, huduma zote zinazohusu masula ya uwekezaji zinaratibiwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania, ambapo Mwekezaji anapata huduma zote kwa wakati mmoja.
https://www.youtube.com/watch?v=lkOWNGlhgWQ&feature=youtu.be
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, ambapo Mbunge wa Viti Maalumu Jacqueline Msongozi alitaka kufahamu hatua zilizochukuliwa na Serikali ili kupunguza urasimu kwa Wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, pamoja na kuweka huduma zote kwenye Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Serikali pia imeandaa mpango wa uwekezaji nchini (Blue Print) ambao utaanza kutumika hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Spika wa Bunge, – Job Ndugai ameitaka serikali kupeleka Bungeni sheria ya Blue Print katika mkutano ujao wa Bunge kama ilivyoahidi, ili mpango uingie kwenye utekelezaji kwa haraka.
