ais John Magufuli amemteua Dkt
John Ndunguru kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa, uteuzi wa Dkt Ndunguru umeanza Septemba Tisa mwaka huu.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Profesa Antony Mshandete kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).
Profesa Mshandete ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ubunifu), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) iliyopo mkoani Arusha.
Uteuzi wa Profesa Mshandete nao umeanza Septemba Tisa mwaka huu.
