Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekabidhi rambirambi ya Shilingi Laki Tano kwa familia ya Christopher Rupia, ambaye ni shabiki wa soka, aliyefariki Dunia baada ya kupata mshtuko wakati wa mchezo kati ya Tanzania na Burundi Septemba 8 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Fedha hizo zimekabidhiwa kwa familia ya Marehemu Rupia huko Ukonga, Mongo la Ndege jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao.
Katika mchezo huo, timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) ilipata ushindi penati 3-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Burundi na hivyo
kutinga hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022.
