Homera awaonya wapotoshaji kuhusu chanjo

0
156

Mkuu wa mkoa wa Katavi, – Juma Homera amewaonya baadhi ya viongozi wa Kidini, Kimila pamoja na wale wa Tiba Mbadala mkoani humo, kutojihusisha na upotoshaji wa makusudi kuhusu chanjo dhidi ya Surua na Rubella, ambazo zitaanza kutolewa kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi Tisa hadi miaka mitano.

Chanjo hiyo itaanza kutolewa kuanzia Septemba 26 hadi 30 mwaka huu.

Homera ametoa onyo hilo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa, baadhi ya viongozi wa aina hiyo wamekua wakipotosha kwa makusudi kuhusu ufanisi wa chanjo hizo.

Mkuu huyo wa mkoa wa Katavi amesisitiza kuwa, yeyote atakayebainika kujihusisha na upotoshaji huo, atachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa atakua amefanya uhalifu.