Kaseja akabidhiwa kitita cha Shilingi Milioni Kumi

0
902

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, – Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars), leo amemkabidhi Mlinda Mlango wa timu hiyo
Juma Kaseja kitita cha Shilingi Milioni Kumi, ikiwa ni sehemu ya motisha na zawadi kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa mchezo baina ya Tanzania na Burundi.

Makonda amemkabidhi Kaseja fedha hizo mbele ya Kocha wa Taifa Stars, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na baadhi ya wachezaji waliomsindikiza.

Akikabidhi fedha hizo, Makonda ameipongeza Stars kwa kutinga hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2022.

Kwa upande wake Mlinda mlango huyo wa timu ya Taifa Juma Kaseja amemshukuru Makonda kwa kutimiza ahadi aliyoitoa ndani ya masaa machache na kuongeza kuwa fedha hizo zitamsaidia katika mambo mbalimbali.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Tanzania iliibuka na ushindi wa penati 3 – 0 dhidi ya timu ya Burundi ambapo mlinda mlango huyo alifanikiwa kupangua mkwaju wa Penati.