Tetemeko la ardhi latokea mkoani Katavi

0
164

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.5 katika kipimo cha matetemeko ya ardhi, – Richta, limeyakumba baadhi ya maeneo mkoani Katavi usiku wa kuamkia hii leo, na kusababisha Wakazi wa maeneo hayo kukimbilia nje ya nyumba zao.

Tetemeko hilo lililotokea saa 9 na dakika 39 usiku, linaelezwa kudumu kati ya muda wa dakika Mbili na Nne na Nusu.

Habari zaidi kutoka mkoani Katavi zinaeleza kuwa, athari zilizosababishwa na tetemeko hilo la ardhi bado hazijafahamika.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwaka huu kwa tetemeko la ardhi kutokea mkoani Katavi, ambapo kwa mara ya kwanza ilikua mwezi June.