Serikali kupunguza kodi vifaa vya madini

0
2014

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema serikali inaangalia uwezekano wa kupunguza kodi katika vifaa na mitambo ya kuongeza thamani ya madini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kushawishi wadau mbalimbali kuwekeza katika uongezaji thamani ya madini hapa nchini.

Akizungumza jijini Arusha alipotembelea kituo cha Jemolojia (TGC) kinachotoa mafunzo ya ukataji na ung’arishaji wa madini, Nyongo amesema lengo la serikali ni kuhakikisha madini yanapata thamani hapa nchini,  hivyo ni vema kituo hicho kikaongeza juhudi ya kuzalisha wataalamu ili waweze kutumika katika uwekezaji huo.