Dkt Shein awafunda Wanahabari

0
171

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, ametoa wito kwa Waandishi wa Habari nchini kuandika habazi zenye mtizamo wa kudumisha amani na utulivu nchini, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Rais Shein ametoa wito huo Kisiwani Unguja,  wakati akifungua mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanachama wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC) na kuongeza kuwa kalamu za Waandishi wa Habari zina nafasi kubwa ya kudumisha amani na utulivu wa nchi.

Ameziagiza Wizara na Taasisi mbalimbali nchini, kushirikiana na Waandishi wa Habari na kuwapatia taarifa pale wanapozihitaji, ili nao waweze kuzifikisha kwa jamii.

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo, Waziri wa Habari, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, – Mahmoud Thabit Kombo, ameupongeza Umoja huo wa Wananchama wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini kwa kuwa umekua ni moja ya njia za kudumisha Muungano.

Akitoa taarifa fupi ya mkutano huo, Rais wa UTPC Dogratius Nsokolo amesema kuwa, Umoja huo umefanikiwa kuwaunganisha Waandishi wa Habari nchini ambao wamekua wakisaidiana katika masuala mbalimbali.